Habari

Madarasa yatumika kufugia Kuku kisa CORONA, Kenya

Uamuzi wa Kenya kufunga shule zote hadi Januari mwakani ili kudhibiti maambukizi ya corona imewaathiri wengi waliokuwa wakifanya kazi katika shule za kibinafsi kama wanavyoripoti waandishi wa BBC Basillioh Mutahi na Mercy Juma.

Wamiliki wa shule ya Brethren wamebadilisha madarasa ya shule ili kufuga kuku

Madarasa katika shule ya Mwea Brethrenl, ambayo yalitambulishwa na sauti za wanafunzi wakisoma, sasa yamejaa sauti za kuku.

Ubao wa darasa uliokuwa umeandikwa muongozo wa kufanya hesabati sasa umebadilishwa na muongozo wa chanjo.

Joseph Maina, ambaye ni mmiliki wa shule nchini Kenya, amegeukia ufugaji wa wanyama ili kujipatia kipato ambacho hawezi tena kupata kutokana na huduma ya kutoa elimu.

‘Muhimu kwa maisha’

Hali ilikuwa ngumu kwake hasa mwezi Machi, wakati shule zilipofungwa, kwasababu alikuwa bado analipa mkopo, na alilazimika kushauriana tena na benki kuhusu namna ya kulipa.

Mwanzoni, kila kitu kilionekana kimesambaratika, lakini “tuliamua kujikakamua kufanya kitu [shuleni] ili tuweze kuishi”, Bw. Maina aliambia BBC.Chakula kinachopatikana huhifadhiwa katika madarasa

Vifaa vinavyotumiwa na wanafuzi vimesukumwa hadi upande mmoja katika shule ya Mwea Brethren ili kutoa fursa ya kilimo

Shule nyingi za kibinafsi ambazo zinaendeshwa kupitia karo inayotozwa wanafunzi, zililazimika kufungwa kwasababu zilishindwa kuwalipa wafanyakazi wake kwasababu baadhi ya shule hizo zinakabiliwa na changamoto za kifedha.

Idadi ndogo ya shule hizo zimeendelea kutoa mafunzo kupitia mtandaoni, lakini fedha wanazopata haziwezi kukidhi mahitaji ya waalimu, kwa mujibu wa chama cha Waalimu wa Shule za Kibinafsi nchini Kenya.(KPSA).

Karibu asilimia 95% ya zaidi ya wafanyakazi 300,000 wa shule za kibinafsi wamepewa likizo ya bila malipo, Afisa Mkuu Mtendaji wa KEPSA, Peter Ndoro anasema.

Kando na hayo shule 133, zimelazimika kufungwa kabisa.

‘Hali haijawahi kuwa mbaya hivi’

Ili kujiepusha na kuchukua hatua kama hizo, shule ya msingi ya Roka, shule nyingine katika eneo la kati nchini Kenya, pia imegeuza majengo yake kufanya shughuli za kilimo.

“Hali haijawahi kuwa mbaya hivi,” James Kung’u, mwanzilishi wa shule hiyo miaka 23 iliyopita, aliiambia BBC.

Nje ya shule hiyo mboga zilizopandwa zinaendelea kukua katika uwanja wa kucheza unaotumiwa na wanafunzi.Uwanja wa kuchezea wa shule ya msingi ya Ronga umebadilishwa na kuwa shamba la mboga

Uwanja wa kuchezea wa shule ya msingi ya Ronga umebadilishwa na kuwa shamba la mboga

Yeye pia anafuga kuku.

“Hali yangu ni sawa na ya shule zingine. Najikakamua kimaisha. Waalimu na wanafunzi hawapo tena hapa. Tumeathirika sana kisaikolojia” Bwana Kung’u anasema.

Shule zote mbili za Mwea Brethren na Roka zimesalia na wafanyakazi wawili, ambao wanasaidia na kufanya kazi ya shamba.

“Sio kazi ya kujitajirisha. Lakini tunashukuru… walau tunajifariji , ukiwa na la kufanya unaondokewa na mawazo,” anasema bwana Kung’u.

Hakuna jukumu la mwalimu

Wakati shule hizo mbili zimejitafutia njia mbadala ya kipato, wamiliki wanahofia hali ya waalimu wao ambao wamekuwa bila mishahara kwa miezi mitano.

Hii ni tofauti na waalimu walioajiriwa katika shule za umma, ambao wamekuwa wakipokea mishahara yao.

Bwana Maina anasema baadhi ya waalimu wanampigia simu kuulizia kazi yoyote. “Lakini kwa bahati mbaya tunapata kidogo tu cha kujikimu sisi wenyewe,” anasema.

Kutokana na changamoto hizo, watu wengi wamegeukia kazi mbadala.

Macrine Otieno, aliyekuwa amefunza katika shule ya kibinafsi kwa miaka sita jijini Nairobi, alifungiwa nyumba baada ya kushindwa kulipa kodi.

Aliamua kufanya kazi ya ndani nyakati za mchana ili aweze kupata pa kuishi na chakula.

“Tangu tulipopata mgonjwa wa kwanza wa corona nchini Kenya, na shule kufungwa, sijakuwa na la kufanya.

“Nimekuwa nikijaribu kujikakamua kufanya kazi za hapa na pale kuwalea wanangu, lakini hali haijakua rahisi,” aliiambia BBC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents