Madawa na bidhaa za viwandani ni hatari

Wananchi wametakiwa kutotumia vibaya madawa na bidhaa zitokazo Viwandani pamoja na Viwatilifu, kwani vinaweza kusababisha madhara makubwa kwa Binadamu na Mazingira.

Wananchi wametakiwa kutotumia vibaya madawa na bidhaa zitokazo Viwandani pamoja na Viwatilifu, kwani vinaweza kusababisha madhara makubwa kwa Binadamu na Mazingira.

Naibu katibu Mkuu kutoka Wizara ya Chakula Kilimo na Ushirika, Bi Sophia Kaduma ameyasema hayo leo katika Mkutano wa Siku mbili wa Wadau wa Chakula na Mazingira wanaopitia Mkakati wa Kitaifa wa Utekelezaji wa Mkataba wa Rotterdam Jijini Dar es Salaam.

Bi. Sofia Amesema Kuwa, Matumizi ya Madawa ya kuuwa wadudu yanaongezeka kutokana na kukuwa kwa Viwanda, na shughuli za Kilimo kwani, dawa hizo hutumika zaidi kuuwa wadudu na ndege kama vile kweleakwelea ambao hushambulia na kuharibu mazao.

Aidha, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Angeline Madete amesema, Madawa hayo yana Athari kubwa kwa Mazingira na Binadamu hivyo kutokana na kuwepo kwa matumizi ya baadhi ya madawa ambayo muda wa mwisho wa matumizi ya madawa hayo yamekabia yaani (Expire date), kuna haja na kila sababu ya kuwa makini zaidi katika matumizi ya madawa hayo.

Mkutano huo wa kwanza Kufanyika Nchini, Umeandaliwa na Idara ya Mazingira ya Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (UNFAO), kinahudhuriwa pia na Wadau kutoka Mazingira Zanzibar, Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, NGOs na Mamlaka ya Mapato Tanzania.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents