Burudani

Madee adai Tekno ni ziada katika muziki wake

Msanii wa muziki Bongo kutoka Tip Top Connection, Madee amesema haamini kufanya ngoma na msanii mkubwa au maarufu ndio kutusua.

Madee ambaye hivi karibuni alitoa wimbo ‘Sikila’ aliomshirikisha Tekno kutoka nchini Nigeria ameeleza kuwa kolabo hiyo imekuja kuongeza baadhi ya vitu katika muziki wake na siyo kwamba alifanya hivyo ili kutusua kimataifa.

“Ambacho hawatakiwi kukiweka moja kwa moja kichwani kwamba ukifanya ngoma na mwanamuziki mkubwa au anayetambulika sana ndio kutusua, hicho kitu kwenye ubongo wangu hakipo kabisa,” Madee ameiambia Bongo5.

“Mimi kutusua ambayo naiamini cha kwanza ni mimi mwenyewe ni tusu?, nikishajua hilo then wewe ambaye nakushirikisha wewe ni ziada tu labda nilikuwa nataka chohote kutoka kwako,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents