Burudani

Madee atoafundisho hili kwa wasanii wenzake

By  | 

Msanii kutoka Tip Top Connection, Madee amefunguka na kusema sababu ya wimbo wake ‘Kazi Yake Mola’ kuendelea kudumu kwa kipindi chote ni kwa sababu kipindi cha nyuma wasanii walikuwa makini katika uandishi na kuingia ndani zaidi katika mada husika, na kuwataka wasanii wa sasa kuiga hilo.

Madee

Akizungumza na East Africa, Radio Madee amesema nyimbo walizokuwa wanatoa wao miaka ya nyuma ziliweza kudumu kwenye chati za muziki kwa kipindi kirefu ukilinganisha na sasa.

“Ninadhani hii iwe kama fundisho kwa marafiki ambao wanaendelea kuandika, nyimbo ambazo zilikuwa zinatoka zamani naamini zimeishi kwa muda mrefu sana, zilikuwa zinakaa kwenye chati kwa kipindi kirefu sana lakini siku hizi nyimbo itatoka leo baada ya siku kadhaa utakuta inaanza kuondoka kwenye chati.

“Kwa hiyo hii ni kitu ambayo inaonekana zamani tulikuwa tuko buys sana, tulikuwa tunaandika sana, tupo deep sana tofauti na sasa hivi tunafanya easy, mtu anaenda studio hana mashairi wala nini, anakaa pale kwenye maiki anaandika,” amesema Madee.

By Peter Akaro

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments