Burudani

Madee awachana wanaomfuatilia Dogo Janja

Mashabiki wengi, wamekuwa wanachukizwa na aina ya malezi ya Madee kwa msanii Dogo Janja kwa muda mrefu. Rapper huyo ameamua kufunguka kuhusu kelele hizo zinazomuandama.

Baadhi ya vitu vinavyodaiwa kutafsiriwa kama malezi mabaya kwa msanii huyo ni pamoja na kutumia fedha vibaya, ikiwemo kumnunulia magari mapya kila kukicha. Akiongea na kipindi cha Dj Show cha Radio One, Madee amesema mtu akilia sana wakati wa kutafuta na akifanikiwa kupata lazima afurahie.

“Kuna muda mtu umelia sana, kwa hiyo inapotokea time ya kufanikiwa kile kitu ambacho ulikuwa unakifukuzia ni heri ya kukifurahia. Nadhani hii ndio nafasi ambayo yupo nayo Dogo Janja sasa hivi, anafurahia maisha yake kwa sababu ya zile hustle zake za kipindi cha nyuma. Hao wanaojaribu kusema kwamba anabadilisha magari, namlea vibaya sijajua ni kina nani na wanataka nini wakati anahangaika kipindi hicho hakuna hata aliyejaribu kumuinua ili kumsaidia,” amesema Madee.

Rapper huyo ameongeza, “Hili sishangai sana ni kawaida ya binaadamu pale unapoona mwenzio anafurahia maisha yake au kitu chochote kile kizuri ambacho amekifanya basi yule aliyekuwa pembeni ananuna.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents