Burudani

Madee: Hip Hop ya Bongo imepooza, hakuna ushindani na ubunifu wa mashairi

Madee amedai kuwa muziki wa hip hop Bongo kwa sasa hivi umepooza tofauti na ilivyokuwa zamani.

Rapper huyo amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio One kuwa zamani msanii akitoa nyimbo lazima kuna msanii mwingine atatokea kumjibu tofauti na ilivyokuwa sasa wasanii wengi wamekuwa wakiachia nyimbo nyingi za mapenzi.

“Kinachokosa kwenye muziki wa hip hop na kimepoozesha ni ule ushindani na ubunifu pia wa mashairi. Unajua hip hop ilivyo asili yake ni majigambo mengi, sasa unapojigamba mbele ya mwenzio halafu yeye anapokuwa amenyamaza tu basi hakutokuwa na ushindani kwa sababu mwisho wa siku itakuwa inaonekana ya kawaida tu,” amesema Madee.

“Kwahiyo zile bifu za hapa na pale siyo zakufuatana na mavisu nyumbani hapana ila kuna bifu fulani zilikuwaga za kibiashara. Labda nikupe mfano zamani East Coast pamoja na TMK ilikuwa bifu fulani hivi zuri kinoma la kibiashara,” ameongeza.

“Ukisikia Jay Moe anatoa nyimbo, Solo Thang anatoa nyimbo basi hapo ujue hapo kuna mtu hapo atakuja atajibu ule wimbo kwa mashairi na kibiashara. Lakini hiyo sasa hivi hakuna watu wanaimba sana mapenzi , watu wanaimba sana nyimbo laini ndio maaana unakuta hakuna ule mvutano kwahiyo game inakuwa inapooza.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents