Burudani

Madee kwa mke wa Roma – Mlitaka na mimi nitekwe?

By  | 

Mke wa Roma Mkatholiki, Nancy Mshana, ameonekana kukerwa na kauli ya Madee aliyoiandika kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Naye kupitia mtandao huo, Nancy aliweka picha akiwa na mumewe na kuandika, “Be a friend. Encourage someone. Take time to care. Let your words heal and not wound. #HusbandSuit by @ki2pe.”

Hapo ndipo Madee alipoibuka na kucomment kwa kuandika, “Apone bas na yy asijilegeze kha!! Wanaume wa Tanga bana @mrs_roma2030.”

Ndipo mrembo huyo wa Roma alipomjibu kwa hasira kwa kuandika kwenye mtandao huo, “@madeeali Nimewaona marafiki na baadhi ya wasanii wakija kumuona, nilitegemea ww ungekuwa wa kwanza kuja kumuona rafiki yako,ndugu yako,mtani wako, lakini huu ni mwezi umekatika sijaona hata ukimpigia simu! Wala kuja kumjulia hali, Hakika nimejifunza mengi sana kipindi hiki, Ubarikiwe sana shemeji yangu Hamad, msalimie mtoto wetu Saida. @madeeali.”

Naye Hitmaker huyo wa Hela, hakuchoka alicomment tena kwa kuandika, “Mlitaka namimi nitekwe @mrs_roma2030.”

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments