Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Madee: Sifahamu mahusiano ya Dogo Janja na Irene Uwoya

Msanii wa Bongo Flava, Madee amekanusha taarifa zinazoenezwa kuwa Dogo Janja alikuwa Mwanza na Irene Uwoya.

Akiongea kupitia U-Heard ya Clouds Fm leo, Madee ameeeleza hana taarifa kuwa msanii wake Dogo Janja alikuwa Jijini Mwanza akiwa amefungiwa chumbani na mwigizaji wa filamu Bongo Irene Uwoya.

‘Ninavyojua mie ni mtu na rafiki yake, sijawahi kuwaona wakija pamoja home ila anasikia kama unavyosikia wewe kuwa ni wapenzi, ila taarifa hizo hazipo rasmi pia nitafatilia kujua kuhusu suala hilo ila hata ikiwa kweli kwani kuna tatizo?,” ameongea Madee.

Na Laila Sued

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW