Madereva teksi wajipanga kudhibiti ujambazi

CHAMA cha Madareva Teksi Tanzania (TG), kimeandaa stakabadhi maalum za teksi kwa lengo la kukabiliana na vitendo vya uhalifu, ujambazi na unyang�anyi vinavyofanywa na baadhi ya madereva wa magari hayo dhidi ya abiria.

Na Kizitto Noya


CHAMA cha Madareva Teksi Tanzania (TG), kimeandaa stakabadhi maalum za teksi kwa lengo la kukabiliana na vitendo vya uhalifu, ujambazi na unyang�anyi vinavyofanywa na baadhi ya madereva wa magari hayo dhidi ya abiria.


Mwenyekiti Mtendaji wa chama hicho, Charles Chembe, alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa stakabadhi hizo mpya zitawezesha kuyabaini magari na madereva wenye tabia ya kuwapora abiria mali zao na kuwafikisha mbele ya sheria. �Kwa kuzingatia matatizo hayo, Tunawajali Group tumeandaa vitabu vya risiti vyenye maelezo yote muhimu kuhusu gari husika, dereva na mmiliki wake,� alisema Chembe.


Alisema risiti hizo zilizotengenezwa kwenye vitabu maalum zikiwa na jina la dereva, kituo chake cha kazi, namba ya kitambulisho chake na namba ya gari zitamwezesha abiria kufuatilia madereva wenye tabia ya kuwapora abiria na kuwafikisha mbele ya sheria.


Alisema wateja wa jiji la Dar es Salaam wanatakiwa kuwasiliana na ofisi za TG kwa namba zilizoko kwenye risiti hiyo huku wateja wa mikoani wakitakiwa kupiga namba za vituo vya teksi kwa msaada huo. �Tunaamini hatua hiyo mpya itapunguza usumbufu na kulinda heshima na kujenga uaminifu kwa wateja wa teksi� alisema.


Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents