Habari

Madereva wa mabasi yaendayo kasi wagoma

Madereva wanaoendesha mabasi yaendayo kasi (UDART), jana walifanya mgomo kwa madai kuwa mishahara wanaolipwa ni midogo na haikidhi mahitaji yao.

31

Mabasi hayo yanatakiwa kuanza kazi kila siku kuanzia saa 11 alfajiri mpaka saa 5 usiku na kila gari likiwa na madereva wawili huku kila mmoja akitakiwa kufanya kazi kwa masaa nane kwa siku.

Mkurugenzi Mkuu wa mradi huo [UDART], David Mgwassa amesema kuwa madereva 30 ambao hawajasaini mikataba ndiyo waliofanya mgomo huo na wengine 300 tayari wameshasaini mikataba yao na wanaendelea na shughuli kama kawaida.

Aidha Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa madereva wanatakiwa kulipwa Sh 800,000 lakini mshahara huo umegawanyika mara mbili ambako kuna Sh 400,000 ambazo hulipwa kila mwezi na kiasi kingine cha Sh 400,000 hulipwa kwa kuangalia kutimizwa kwa vigezo vya masharti ya mkataba.

“Shilingi 400,000 ni kiwango kisichobadilika kwa mwezi lakini baada ya kupimwa vigezo sita ambavyo ni usafi, kuwahi kazini, kutopata ajali na kuwahi kwa wakati kutoka kituo kimoja hadi kingine ndiyo hulipwa Sh 400,000 nyingine,” alisema Mgwassa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents