BurudaniHabari

Madinda kuingia School

Aisha MadindaMsichana anayeaminika kuwa na mvuto kuliko mabinti wengi tu hapa jijini na anayesifika kwa kuyakata masebene kwa umahiri wa hali ya juu bi Aisha Madinda, hivi karibuni amefikia uamuzi wa kwenda shule kwa ajili ya kujipatia ujuzi wa ziada..

Aisha MadindaMsichana anayeaminika kuwa na mvuto kuliko mabinti wengi tu hapa jijini na anayesifika kwa kuyakata masebene kwa umahiri wa hali ya juu bi Aisha Madinda, hivi karibuni amefikia uamuzi wa kwenda shule kwa ajili ya kujipatia ujuzi wa ziada pasi na kuitegemea kazi yake hiyo ya unenguaji inayompatia riziki.

Akizungumza na mwandishi wa Bongo5 alipozuka kwenye ofisi hizo Mamaa Madinda alisema “katika maisha kuna leo na kesho sitarajii kuwa mcheza show katika maisha yangu yote na ndio maana naiheshimu sana kazi yangu hii kwani inaniwezesha kupata rasilimali ambazo naamini zitanisaidia hapo baadae kimaisha.

“nimefikia uamuzi wa kwenda shule baada ya kukaa na kufikiria kuwa, iwapo nitachoka kuwa mcheza show ni kazi gani ambayo nitafanya ili kusonga na maisha? Jibu pekee na la karibu lililonijia ni shule kwanza ndio naweza kujua nini la kufanya baada ya hapo” alisema Binti huyu.

Hivi sasa yuko mbio ile mbaya kutafuta chuo kwa ajili ya kujipatia mafunzo ya kompyuta katika levo ya juu na sio viwango vya awali kama wafanyavyo wengi kwani matarajio yake ni kustaafu masuala ya unenguji katika kipindi ambacho washabiki wake watakuwa bado wakimuhitaji “nisingependa kuwa na historia mbaya kwani huko nilikotoka nimekuwa nikijiheshimu sana sasa sitaki kujiharibia”-Madinda.

Source: Bongo5

{mos_sb_discuss:6}


Bongo5.com brings you the latest news from East Africa at your finger tips. If you have a story you’d like to share please send an email to [email protected]

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents