Habari

Madonna Aikera Serikali ya Malawi


Mwanamuziki mwenye umri mkubwa lakini bado anazidi kudai kwenye anga za Muziki na Dance, Madonna, Karibuni ameikera serikali ya Malawi kwa kutotekeleza ahadi za kujenga shule nchini humo, na kudai kubadilisha mfumo wa kutoa msaada huo wa kielimu.

Madonna ambaye ameachia albam yake ya umi na moja inyoenda kwa jina la MDNA, alimchukua mtoto wa kimalawi kwa jina la David Banda na kumpa makazi nyumbani kwake na kumpeleka shule. Baada ya kitendo hicho, Madonna aliahidi kujenga shule kwa ajili ya watoto wa kike wasiojiweza nchini humo.

Baada ya muda mrefu kupita, Serikali ya Malawi imeshangazwa kwa kutotekelezwa kwa ahadi hizo na pia kwa upande wa Madonna kubadili kujenga shule na kuamua kutoa pesa kuendeleza shule ambazo tayari zipo, hivyo kukiuka utaratibu wa mkataba walioafikiana.

Madonna katoa ‘No Comment’

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents