Burudani

Madonna amtabiri mwanaye kuwa Rais wa Malawi

Malkia wa muziki wa Pop kutoka Marekani, Madonna Louise Ciccone maarufu kama Madonna amemtabiria kijana wake wa kiume kuwa Rais.

Madonna ametoa utabiri huo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter ambapo ameandika kuwa kijana wake wa kiume David Banda (12) anatakuja kuwa rais wa Malawi.

“On President’s Day I celebrate The Future President of Malawi! The Warm Heart of AfricA. #banda #destined #for #greatness .”

Mnamo mwaka jana msanii huyo aliweza kuwaasili watoto wawili mapacha ambao ni Esther na Stella Mwale. Kwa idadi hiyo Madona ana jumla ya watoto sita huku wane wakiwa wa kuwaasili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents