Habari

Maduka 816 ya dawa yanyang`anywa leseni

Maduka 816 ya kuuza dawa baridi jijini Dar es Salaam, yamenyang anywa leseni za kufanya biashara hiyo, kutokana na kutokuwa na wauza dawa wenye taaluma hiyo.

Na Joseph Mwendapole

 
Maduka 816 ya kuuza dawa baridi jijini Dar es Salaam, yamenyang�anywa leseni za kufanya biashara hiyo, kutokana na kutokuwa na wauza dawa wenye taaluma hiyo.

 

Kadhalika, wamiliki wa maduka ya dawa baridi ambao hawana vibali, wameagizwa kusitisha biashara hiyo mara moja.

 

Agizo hilo lilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Abbas kandoro, kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri wa Dawa ya Mkoa wa Dar es Salaam.

 

Mkutano huo ulihusu utoaji wa vibali vya kuendesha biashara ya dawa baridi kwa mwaka 2006/7.

 

Alisema watakaokiuka agizo la kusitisha biashara hiyo watafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

 

Bw. Kandoro alisema Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwa kushirikiana na Manispaa za Ilala, Kinondoni na Temeke zilifanya ukaguzi wa majengo yaliyoombewa vibali vya kufanya biashara hiyo mwaka jana.

 

Alisema maduka 1, 393 yalikaguliwa ambapo kati ya hayo maduka 577 ndiyo yalipewa vibali vya kuendelea na biashara hiyo.

 

Alisema kuanzia mwaka 2,000 mpaka sasa kumetokea mfumuko wa maduka ya dawa baridi hasa katika maeneo ya mijini kinyume na malengo yaliyotarajiwa.

 

Alisema ukaguzi uliofanywa unaonyesha kuwa asilimia 54 ya maduka yaliyokaguliwa hayakuwa na vibali vya kuuza dawa hizo na asilimia 95 hayakuwa na wauzaji wenye taaluma ya dawa.

 

Alisema asilimia 99 ya maduka hayo yalikutwa yakiuza dawa baridi na moto, bandia na dawa ambazo ubora wake haujahakikiwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA.

 

Aidha, alisema maduka 18 yalikutwa yakitoa huduma za tiba pamoja na vifaa vya hospitali kama vile vifaa vya kutolea mimba, na vifaa vya kutahiri.

 

Bw. Kandoro alisema asilimia 43 ya maduka mengine yalikutwa yakiwa katika majengo yasiyokidhi viwango vya kuendeshea biashara ya dawa baridi.

 

Alitoa mfano kuwa baadhi ya maduka hayo yamewekwa kwenye vyumba vidogo na vichafu.

 

Alisema tathmini iliyofanywa inaonyesha kuwepo kwa ongezeko kubwa la ukiukwaji wa sheria unaofanywa na maduka hayo hivyo kuwepo uwezekano wa kuathiri afya za watumiaji.

 

Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents