Habari

Maduka yafungwa kwa muda kuhofia maandamano

Maduka mengi katika soko kuu mkoani Mtwara yamefungwa kwa masaa kadhaa nyakati za asubuhi kwa kile kilichoelezwa na wamiliki wa maduka hayo kuwa ni hofu ya maandamano yaliyokuwa yanaratibiwa mitandaoni, Jambo ambalo limesababisha wakazi wa mji huo kukosa mahitaji muhimu nyakati za asubuhi.

Mmoja wa wafanyabiashara waliofunga maduka yao asubuhi ya leo, Ibrahimu Kaseka alipoulizwa na kituo cha runinga cha ITV amesema kuwa amechukua hatua hiyo muda wa asubuhi kwa kutokana na vugu vugu la maandamano ila kwa sasa amefungua baada ya kuona doria kuimarishwa na askari polisi katika soko hilo.

Hata hivyo, tayari usafari wa daladala, huduma za kijamii zimerudi katika hali yake ya kawaida mjini Mtwara baada ya hofu ya maandamano kupotea.

Naye Kamanda wa Polisi mkoani Mtwara, Kamishna Msaidizi wa Polisi Lucas Mkondya amesema kuwa hali kwa sasa mkoani Mtwara ipo poa na wananchi wanaendelea na majukumu yake kama kawaida, huku akithibitisha kuwa jeshi hilo linawashikilia wanafunzi wawili wa Chuo cha SAUT tawi la Mtwara kwa kuchochea maandamano mitandaoni.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents