Habari

Maelfu ya samaki wanatarajiwa kuokolewa kwa ndege, baada ya kukwama kwenye maporomoko ya ardhi Canada

Maelfu ya samaki wanatarajiwa kuokolewa kwa ndege, baada ya kukwama kwenye maporomoko ya ardhi Canada

Maelfu ya samaki aina ya salmon nchini Canda wanatarajiwa kuokolewa kwa ndege baada ya kukwama mtoni kutokana na maporomoko ya ardhi. Mwezi Juni, maafisa maafisa waligundua kuwa miamba iliyoshushwa na maporomoko imeziba kipande cha mto Fraser katika jimbo la British Columbia, na kuwazuia maelfu ya samaki hao kuelekea juu ya mto ambao hutaga mayai.

Kwa mujibu wa BBC. Vikosi vya uokozi vimepiga kambi katika eneo hilo kupanga mkakati wa namna ya kuwaokoa samaki hao kwa kuwasafirisha mpaka upande wa pili wa mto kwa kutumia helikopta.

Watunza mazingira wametoa tahadhari kuwa inabidi kila liwezekalo lifanyike ili samaki hao watage mayai ama la idadi yao itapungua na kuwa hatarini.

Haijulikani ni samaki wangapi ambao wamenasa, lakini inaaminika kuwa ni 700 tu ambao wameweza kuvuka kikwazo hicho bila ya msaada wowote.

The site of the rock slideHaki miliki ya pichaPROVINCE OF BRITISH COLUMBIA
Image captionMaporomoko ya ardhi yamezuia njia za samaki toka mezi Juni katika mto Fraser

Makabila mengi ya asili nchini Canada wanategemea samaki hao kama chakula na bidhaa muhimu kwenye sherehe zao za jadi.

Waziri wa uvuvi wa Canada, Jonathan Wilkinson, amesema serikali imekuwa ikifanya kazi usiku na mchana kuwasaidia samaki hao.

Hata hivyo bado haijatangazwa tarehe rasmi ambapo uokozi huo wa kutumia ndege utafanyika.

Vikosi vya uokozi kwa sasa vinatengeneza bwawa la kuwazuia samaki hao.

Baada ya kuelekezwa kwenye bwawa hilo, watawekwa matanki ya lita 780-2,700 na kunyanyuliwa na helikopta kutoka eneo hilo la maporomoko.

Matanki hayo yatapuliziwa hewa ya oxygen ili kuwasaidia samaki watulie na kufika salama.

Workers create a tank for the fishHaki miliki ya pichaPROVINCE OF BRITISH COLUMBIA
Image captionVikosi vya uokozi bado vingali kazini kuwanasua maelfu ya samaki nchini Canada

Wakati bwawa hilo likitengenezwa, maafisa sasa wanafunga vifaa maalum baadhi ya samaki hao ili kufuatilia myenendo yao baada ya kuokolewa.

Vikosi hivyo pia vinaendelea na kazi ya kuondoa mawe makubwa yaliyozuia eneo hilo ili hapo baadae samaki waweze kupita wenyewe pamoja na mawe makubwa mengine ambayo yanaweza kuhatarisha maisha ya watu.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents