Tupo Nawe

Maelfu ya wanaume waliyokuwa nusu utupu wawania fimbo ya bahati Japan

Maelfu ya wanaume waliokuwa nusu uchi wanagombania fimbo mbili katika tamasha lililofanyika Japan.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la BBC, Wanaume elfu kumi waliovalia vinguo vyeupe walishiriki katika sherehe katika nyumba maalum.

Saidaiji-eyo festival

Washiriki walipambana kwenye maji ili kutafuta fimbo ambazo zilikuwa zimerushwa katika umati wa watu.

Wale waliopata fimbo zenye urefu wa sentimita 20, zinaitwa”shingi”, wanaaminika kuwa ndio wanaume wenye bahati zaidi mwaka huu.

Saidaiji-eyo festival

Maadhimisho haya yalikuwa ya 510 katika historia ya Japan.

Maelfu ya washiriki hawa uoga maji ya baridi katika mto Yoshii ili waweze kutakaswa kabla hawajaanza kutafuta fimbo ya bahati.

Saidaiji-eyo festival

Mara baada ya kumaliza kuoga maji hayo baridi, taa huwasha.

Mkuu wa sehemu hiyo ya kuabudia husimama juu kwa mita nne na kurusha fimbo hizo mbili katika mkusanyiko mkubwa wa watu.

Watu wawili watakaoweza kuzipata fimbo hizo hutajwa kuwa washindi wenye bahati.

Saidaiji-eyo festival

Tamasha la ‘Saidaiji-eye’ ni miongoni mwa matamasha makubwa katika tamaduni za Japan katika kalenda ya mwaka.

Vilevile tamasha hili linafikiriwa kuwa linaleta mazao mazuri katika mwaka.

Saidaiji-eyo festival

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW