Habari

Maendeleo: Matatu za Kenya zaenda digital, sasa abiria kufaidika na Internet ya bure wawapo safarini

Hakuna muda ambao huwa unakera kwa watumiaji wa usafiri wa jumuiya kama asubuhi wanapokuwa wanaelekea katika shughuli zao na jioni wakiwa wanarejea majumbani mwao, kutokana na msongamano mkubwa wa magari barabarani. Lakini nchi ya Kenya imepiga hatua zaidi kwani sasa wasafiri wanauwezo wa kupata huduma ya internet ya bure katika matatu na mabasi wanapokuwa safarini.

matatu

Hivi karibuni kampuni ya mawasiliano ya Safaricom ya Kenya imeingia ubia na wamiliki wa magari ya abiria ya Kenya maarufu kama matatu na mabasi kwaajili ya kutoa huduma ya internet ya bure katika magari yao, ambapo mpaka sasa tayari matatu zaidi ya 40 zimekwishawekewa Wi-fi na abiria wa Nairobi wameanza kufaidi huduma hiyo.

Taarifa hiyo ambayo imeripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari Kenya imesema, malengo ya Safaricom ni kuweza kufikisha huduma hiyo katika matatu na mabasi yapatayo 200 ifikapo (September) mwaka huu.

Akizungumza katika uzinduzi huo CEO wa Safaricom Collymore, alisema “Most of our customers use matatus and buses as their preferred mode of transport on a day-to-day basis. This therefore presents us with a fantastic opportunity to drive home the Internet story and make it a way of life among our customers whom we believe we will achieve by availing free Wi-Fi internet in matatus,”

Naye mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa matatu Simon Kimutai alisema, sasa watu hawatakuwa bored wanapokuwa katika msogamano wa magari barabarani kwani watautumia muda huo kufanya mambo ya msingi bila gharama yoyote ya ziada. “People will no longer get bored while held up in jam because they can chat through Facebook, tweet and much better students can be doing their research as they go to training centers,”

Ili matatu iweze kufungiwa huduma hiyo inatakiwa kuwa na simu yenye uwezo wa kupata internet na Wi-fi.

Matatu nyingi za Kenya (kama sio zote) zimefungiwa muziki mkubwa pamoja na TV zinazowafanya abiria kutochoka na safari, na sasa huduma ya Internet ya bure imeongeza utofauti katika sekta hiyo ya usafirishaji nchini humo.

Tazama video ya Matatu iliyofungiwa Wi-fi

Source: Capital FM Kenya

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents