Habari

Mafuriko yanavyoendelea kuathiri katika mataifa ya Afrika mashariki, Yaua watu 22 Uganda – Video

Mafuriko yanavyoendelea kuathiri katika mataifa ya Afrika mashariki, Yaua watu 22 Uganda - Video

Mafuriko nchini Uganda yamekatisha maisha ya watu 20, kufuatia mvua kubwa magharibi mwa nchi hiyo. Vikosi vya uokozi vimekuwa katika jitihada za kunasua wale waliokwama kutokana na mafuriko hayo katika wilaya ya Bundibugyo.

Makazi ya watu katika eneo hilo yamesombwa na barabara kadhaa hazipitiki baada ya kuharibiwa vibaya.

Mvua hizo ni mwendelezo katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo zaidi ya watu 200 wamepoteza maisha toka mwezi Oktoba mwaka huu, na takribani watu milioni wamelazimika kuyakimbia makazi yao.

Hali hiyo ya mvua imetokana na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yalikuwa yanatengeneza kimbunga ambacho kilitua pwani ya Somalia mwishoni mwa wiki iliyopita.

Nchini Uganda, mvua ziliimarika na kuwa kali zaidi kuanzia Ijumaa mpaka Jumamosi.

Polisi, wanajeshi, mashirika ya misaada na wasamaria wema kutoka kwenye jamii wanaendelea na zoezi la kuwaokoa watu waliokumbwa na mkasa huo.

Presentational white space

Hali ya Somalia ikoje?

Jimbo la Puntland lilikuwa likijiandaa na kimbunga kilichopewa jina la Pawan, lakini kimbunga hicho kilipungua makali kabla ya kutokea.

Tayari jimbo hilo lilikuwa limeshaathirika kutokana na mvua na mafuriko kabla ya kimbunga kupiga.

Watu wawili wameripotiwa kupoteza maisha, mvuvi mmoja ambaye boti yake ilizama kwa mawimbi makali na mtoto ambaye maji ya mafuriko yalipita kwenye nyumba yao.

Kwa mujibu wa BBC, watu wengi katika jimbo hilo walikimbia makazi yao kabla ya kimbunga hicho kutokea hususani katika mji wa pwani wa Eyl.

Baadhi ya barabara zimeharibiwa vibaya na kufanya mawasiliano ya usafiri kuwa magumu katika eneo hilo.

Maeneo mengi ya ukanda wa Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika yamepata mvua ya zaidi ya asilimia 300 baina ya mwezi Oktoba na katikati ya Novemba.

Djibouti, Ethiopia, Kenya, Uganda, Tanzania, Somalia na Sudani Kusini zimekumbwa na mvua kubwa katika baadhi ya maeneo.

Takribani watu 300 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya milioni 2.8 wameathirika kwa namna moja au nyingine, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents