Habari

Mafuriko yaua watu 7 Dar, Jeshi la polisi latoa tahadhari kwa wazazi na walezi

Kufuatia mvua kali zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam watu 7 mpaka sasa wameripotiwa kupoteza maisha katika maeneo mbali ya jiji la Dar es salaam.

Akiongea na Bongo5, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha taarifa hizo ambapo amesema kuwa watu sita wameripotiwa kufariki katika wilaya za Kinondoni na Ilala huku mmoja akiripotiwa kufariki katika wilaya ya Temeke.

Mpaka sasa tumepokea taarifa za vifo vya watu saba katika maeneno mbalimbali ya jiji la Dar es salaam ambapo watatu wamefariki wilaya ya Kinondoni, wengine watatu wilaya ya Ilala na mmoja umekutwa ukielea katika bonde la mto msimbazi. Hii ni kutokana na mvua kali zinazoendelea kunyesha jijini Dar es saalamu,“amesema kamanda Mambosasa.

Kwa upande mwingine, Mambosasa ametoa tahadhari kwa wazazi na walezi kwa kuwataka kuwa makini na watoto wadogo hasa hasa wanafunzi katika kipindi hiki cha mvua kali zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents