Habari

Magari 22 ya Tanesco yakamatwa

JUMLA ya magari 22 mali ya Shirika la Umeme nchini (Tanesco) yanashikiriwa kwenye kwenye ghala la Kampuni ya udalali la Yono Auction Mart, baada ya shirika hilo kukaidi amri ya Mahakama Kuu iliyowataka kurejesha umeme mara moja kwenye Kiwanda cha Morogoro Canvas Mill Limited (MCML).

na Happiness Katabazi

Magari hayo yanashikiliwa kwenye ghala la kampuni hiyo ya udalali lililopo Keko, Dar es Salaam.

Vyanzo vya kuaminika kutoka mahakamani hapo vinasema tayari Tanesco wameandika barua ya maombi kutaka kurejeshewa magari hayo katika mahakama hiyo na leo asubuhi inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu ombi lao.

Ijumaa iliyopita, Jaji Catherine Orio alikubali ombi la MCML lililokuwa likitaka magari ya Tanesco yakamatwe ili shirika hilo liweze kurejesha umeme kiwandani hapo ambao ulikatwa bila kufuata taratibu.

Uamuzi huo ulikuja ikiwa ni wiki tatu tangu Tanesco kuwasilisha ombi la kulalamikia kampuni hiyo kwamba inajiunganishia umeme wa shirika hilo kinyume cha sheria na ililitaka kiwanda hicho kiilipe sh milioni 606 na mahamaka hiyo mapema mwaka huu ilitoa uamuzi kwamba kiwanda hicho kisikatiwe umeme hadi mahakama itakapomaliza kusikiliza kesi ya msingi.

Jaji Oriyo alisema kuwa mahakama haiwezi kutoa adhabu kwa mtu binafsi kwa kesi kama hiyo, inatoa uamuzi wa kukamatwa mali za Tanesco kama adhabu.

Source: Tanzania Daima

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents