Burudani

Maggie Vampire afunguka alivyopata dili la kufanya video mpya ya Davido

Mrembo wa kupamba video Bongo, Maggie Vampire amefunguka alivyopata dili la kuonekana katika video mpya ya msanii wa Nigeria, Davido.

Akiongea na gazeti la Bingwa, Maggie amesema wakati anapata dili hilo hakuwa anafahamu kama video hiyo itakuwa ya Davido mpaka pale alipofika location kisiwani Zanzibar ndio akafahamu hilo.

“Nilitafutwa nikaambiwa kuna video Zanzibar inatakiwa nikafanye, nikaambiwa nitalipwa bei fulani na mimi nikaridhika nikaenda. Sikujua kama ni Davido, ile nafika tu nakutana na Davido ilikuwa ni surprise kwangu,” amesema mrembo huyo.

“Kiukweli Davido ni mtu poa sana na suala la malipo na malazi yalikuwa mazuri tofauti na wasanii wetu wa Bongo na tulifanya video ile kwa siku mbili,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents