Mahabusu wazua mgomo gerezani

Mahabusu wa Gereza la Keko, jijini Dar es Salaam, jana waligoma kula chakula kwa madai kwamba chakula wanacholishwa ni kibovu kupitilia

Mahabusu wa Gereza la Keko, jijini Dar es Salaam, jana waligoma kula chakula kwa madai kwamba chakula wanacholishwa ni kibovu kupitilia.



Habari kutoka ndani ya gereza hilo zimedai kuwa mahabusu hao walianza mgomo huo jana asubuhi, kwa madai kwamba wamechoshwa kulishwa dona.



“Ni kweli kabisa mahabusu wa Gereza la Keko wamegoma kula chakula kuanzia asubuhi, kwa madai kwamba chakula wanacholishwa hakifai kwa matumizi na afya ya binadamu.



“hapo mwanzo walikuwa wakilishwa sembe lakini ghafla hivi karibuni wameanza kulishwa dona na kwa kweli wana haki ya kugoma kula chakula hicho, kwa kuwa ni kibaya na hakina ladha mdomoni,” alisema mtu mmoja aliyezungumza na mtandao huu jina limehifadhiwa.



Vyanzo kutoka ndani ya gereza hilo, vilibainisha kuwa, mahabusu hao wameapa kuendelea na mgomo wao wa kutokula chakula hicho, hadi uongozi wa gereza hilo utakapowabadilishia mlo wao.



Habari kutoka gerezani humo zilieleza kuwa, mahabusu hao walifanya mgomo huo wakiwa katika hali ya utulivu uliokithiri bila kelele wala fujo, tofauti na ilivyozoeleka hasa wanapokuwa katika kipindi cha mgomo.



Mwaka jana mahabusu kutoka magereza mbalimbali hapa nchini wakiwemo wa Keko, waligoma kushuka kwenye makarandika kwa ajili ya kuudhuria kesi zao katika mahakama mbalimbali nchini, kwa madai kadhaa.



Mahabusu hao walikuwa wakilalamikia kucheleweshwa kwa kesi zao na mlundikano wa mahabusu katika magereza.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents