Moto Hauzimwi

Mahadhi asema haya baada ya bao lake dhidi ya St Louis

Baada ya kumalizika kwa mchezo wa klabu bingwa barani Afrika baina ya Yanga SC ilioyoibuka na ushindi wa bao 1 – 0 dhidi ya  St Lous mfungaji wa bao hilo ambaye ni kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Juma Mahadhi amesema kuwa alikwenda kutimiza majukumu aliyoelekezwa na mwalimu wake.

Mahadhi ameyasema hayo kupitia mahojiano yake na chombo cha habari cha Azam tv.

“Nimefata maelekezo ya mwalimu baada ya kuangalia kitu gani kinakosekana ndani pale na ndicho nilichokwenda kufanya,”amesema Mahadhi.

Juma Mahadhi ameongeza “Naamini tutajipanga vizuri kwa sababu sisi tulikuwa hatuwajui na wana wanaulinzi imara sana naamini tutafanya vizuri mchezo ujao.”

Juma Mahadhi ambaye ni kiungo mshambuliaji ndani ya mabingwa hao wa kihistoria wa ligi kuu soka Tanzania Bara aliingia uwanjani kipindi cha pili akichukua nafasi ya Ibrahim Ajib aliyekwenda benchi.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW