Habari

Mahakama 20 za mwanzo kujengwa Dar

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema serikali ina mpango wa kujenga mahakama 20 za mwanzo katika mkoa wake.


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.

Mkuu wa mkoa huyo amesema hayo alipokutana na waziri wa katika na sheria, Dkt Harrison Mwakyembe Jumatatu hii jijini humo.

“Mimi na wakuu wangu wa wilaya tumemuahidi mheshimiwa waziri kwenye mkoa wetu wa Dar es Salaam,tutajenga mahakama za mwanzo 20 ili kuweka kuongeza kasi ya utoaji na upatikanaji wa haki kwa wananchi endapo wanapelekwa katika vituo vya polisi kupelekwa mahakamani au pale ambapo wanakwenda mahakamani baada ya kukaa maamuzi kwa muda mrefu. Tunategemea kutoka wizarani tutapokea ramani ina muongozo wa vituo viweje na mahakama ziweje,” amesema Makonda.

Hivi karibuni mkuu huyo wa mkoa alileta wanasheria 35 katika mkoa wake watakaotoa msaada wa kisheria kwa wananchi.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents