Habari

Mahakama Kuu yatengua hukumu ya kifungo cha miezi mitano alichotumikia Mhe. Sugu

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya leo tarehe 11 October 2019 imetengua Hukumu, Mwenendo na Kifungo alichohukumiwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi almaarufu Sugu kwa kile ambacho Mahahaka Kuu imeeleza kuwa ni ubatili wa mwenendo katika kesi hiyo.

 

Akisoma Uamuzi wa Rufaa hiyo Nambari 29 ya Mwaka 2018, Iliyowasilishwa na Sugu kupitia Mawakili Peter Kibatala na Faraji Mangula, Jaji Utamwa amesema kwamba kulikuwa na Makosa yasiyotibika katika mwenendo wa shauri hilo, Hasa pale ambapo aliyekuwa Hakimu Mwandamizi Mteite wa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mbeya aliposhindwa kuwasomea Mashtaka Washtakiwa katika hatua ya usikilizaji wa awali (Preliminary Hearing).

Katika Hukumu yake iliyosomwa na Naibu Msajili wa Mahakama wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Jaji Utamwa amesema kuwa hakubaliani na hoja za upande wa Serikali ambao ni ndio Wajibu Rufaa, Kwamba mapungufu hayo yanatibika.

Jaji Utamwa amesema kwamba makosa hayo yanaathiri mwenendo mzima wa kesi iliyopelekea kufungwa kwa Sugu na mwenzake Emmanuel Masonga.

Mwezi Februari mwaka huu, Mheshimiwa Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga walihukumiwa kifungo cha miezi mitano na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents