Habari

Mahakama ya mafisadi kuanza kushughulikia rushwa ndogo ndogo

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Harrison Mwakyembe amesema serikali inatarajia kujadili kushusha kiwango cha fedha kinachohusika katika makosa ya rushwa na uhujumu uchumi kwenye mahakama ya mafisadi ili kukomesha vitendo vya rushwa.

Waziri Mwakyembe alitoa kauli hiyo Jumatatu hii baada ya kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

“Nimeulizwa sana na waandishi wa habari tangu Julai hadi sasa walitegemea kungekuwa na kesi nyingi lakini kuna kesi moja katika Mahakama ya mafisadi tumekuja kubaini kwamba uchache wa kesi ndiyo mafanikio makubwa ya hatua ya kisheria tuliyochukua,” alisema.

“Sisi kama serikali tukiona wizi sasa umeanza kupungua na kuenea katika viwango vya shilingi milioni 400, 500, 700 tumeanza kujadiliana kuangalia uwezekano wa kushusha kiwango cha fedha ili tuweze kukomesha kabisa udokozi, ubadhilifu, wizi wa fedha au mali ya umma,” aliongeza.

Waziri huyo alishukuru uamuzi wa mkuu wa mkoa huo, Paul Makonda kutafuta vijana wanaojua sheria ili kusaidia wananchi kabla ya kwenda mahakamani ni mzuri.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents