Habari

Mahakama ya Rufani yatupilia mbali maombi ya aliyekuwa mkuu wa upelelezi Kinondoni

Mahakama ya Rufani imetupilia mbali maombi ya marejeo ya aliyekuwa Mkuu Upelelezi wa Wilaya ya Kinondoni (OC-CID), Mrakibu wa Polisi (SP) Christopher Bageni aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa.

ImageMwaka 2016, Bageni aliwasilisha maombi ya marejeo mahakamani hapo akiiomba mahakama hiyo ibadilishe uamuzi wake.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Azam Tv, Uamuzi wa kutupilia mbali maombi hayo ya Bageni ulioandaliwa na jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo waliosikiliza maombi hayo, umetolewa leo, Jumatano, Agosti 14, 2019 na Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufani, Elizabeth Mkwizu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents