Habari

Mahakama yapanga tarehe ya kesi ya Nabii milioneaa Bushiri

Mahakama ya juu zaidi nchini Malawi imepanga kusikiliza kesi ya Nabii milionea Shephard Bushiri na mke wake Mary tarehe 1 Disemba.

Katika kesi hiyo waendesha mashitaka watakuwa wakipinga kuachiliwa huru bila masharti kwa Bushiri na mke wake ambao walikwepa kesi ya dhamana nchini Afrika Kusini na kutorokea katika nchi yao ya asili-Malawi wakidai kwamba walikuwa wanatishiwa maisha yao.

Wanakabiliwa na mashitaka ya utakatishaji wa pesa na ufisadi nchini Afrika Kusini.

Kibali cha kuwakamata kilitolewa na serikali ya Afrika Kusini kupitia ushirika wa polisi ya kimataifa-Interpol na wakajisalimisha kwa polisi nchini Malawi ambao waliwakamata na kuwaweka mahabusu kwa usiku mmoja.

Walipelekwa katika mahakama ya hakimu mkazi mjini Lilongwe ambako waliachiliwa huru kwa misingi kwamba kukamatwa kwao hakukufuata utaratibu sahihi.

Mwendesha mashitaka wa serikali alikuwa ameiomba mahakama iwaruhusu polisi kuendelea kuwashikilia wawili hao katika mahabusu kwa siku 30 zaidi, ili kuipatia muda serikali ya Afrika Kusini wa kuwasilisha rasmi ombi la kuwapeleka Afrika Kusini kukabiliana na kesi yao.

Waendesha mashitaka wa Malawi wamekata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents