Habari

Mahojiano ya DCI na Mhe. Lowassa yapigwa kalenda (+Picha)

Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amewasili katika makao makuu ya Jeshi la Polisi leo kama alivyoelekezwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) siku ya Jumanne wiki hii.

Lowassa amewasili akiwa ameongozana na baadhi ya viongozi wengine wa Chadema.

Ofisi ya DCI imemtaka Waziri Mkuu huyo wa zamani kuripoti tena ifikapo Julai 13 kutokana na uchunguzi kutokamilika.Hata hivyo Askari waliwafukuza waandishi wa habari waliokuwa katika eneo hilo na kuwataka kusogea mbali na eneo la makao makuu hayo.

Wakili Peter Kibatala alisema Lowassa alihojiwa kwa kosa la uchochezi kwa kauli yake aliyoitoa Juni 23 na kwamba baada ya kuhojiwa aliandika maelezo ya onyo juu ya kauli yake ambayo inadaiwa ni ya kichochezi.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents