Habari

Mahojiano ya DCI na Mhe. Lowassa yapigwa kalenda tena

Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai(DCI), ametakiwa kurudi tena July 20 bila sababu kuwekwa bayana.

Peter Kibatala ambaye Mwanasheria wa Lowassa, amezungumza na wanahabari amesema Lowassa anatakiwa ametakiwa kurudi Alhamisi. “Hatujaambiwa kwa nini ila tumeambiwa tuje alhamisi ijayo kwa ajili ya maelekezo na kuwasikiliza zaidi.”

Hata hivyo Juni 29, Wakili Peter Kibatala alisema Lowassa alihojiwa kwa kosa la uchochezi kwa kauli yake aliyoitoa Juni 23 na kwamba baada ya kuhojiwa aliandika maelezo ya onyo juu ya kauli yake ambayo inadaiwa ni ya kichochezi.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents