Shinda na SIM Account

Mahusiano ya Alikiba na mrembo wa Kenya yaanza kuvuja, adaiwa ndiye aliyempiku Jokate

Kamera zinazidi kummulika Alikiba. Ukweli wa mahusiano yake na mrembo kutoka mjini Mombasa, Kenya anayefahamika kama Aminah umeanza kufichuka wazi.

Wiki mbili zilizopita Bongo5 tulikuletea stori ya hitmaker huyo wa Seduce Me na mrembo huyo ambao kwa mujibu wa vyanzo vyetu kutoka Kenya vilituambia kuwa walitakiwa kufunga ndoa Machi 2 ya mwaka huu, hata hivyo stori kamili kilichoendelea kuhusu ndoa hiyo hatukuweza kuzipata.

Hata hivyo ukweli wa mahusiano ya wawili hao umeanza kuonekana wazi kutokana na moja ya ujumbe huo hapo juu ambao Alikiba na Aminah walitumiana kupitia mtandao wa Twitter. Kupitia mtandao huo Aminah anatumia jina la AmyRekish.


Picha ya Aminah ambaye anadaiwa kuwa mpenzi wa Alikiba

Kwa mujibu a vyanzo vyetu vimeendelea kumtafuta mrembo huyo na kupata taarifa kuwa anafanya kazi ya Fiscal analyst (Mchambuzi wa masuala ya fedha) kwenye serikali ya kaunti ya Mombasa.

Chanzo hiko kimeendelea kwa kusema kuwa Alikiba na Aminah wameanza mahusiano tangu mwaka 2016 na pia inadaiwa kuwa mrembo huyo ndiye aliyempokonya tonge mdomoni mrembo Jokate Mwegelo ambaye mara kadhaa aliwahi kudaiwa kuwa na mahusiano ya msanii huyo.

Hata hivyo bado tunaendelea kumtafuta Alikiba kwa ajili ya kupata taarifa hizo kiundani zaidi.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW