Maisha Plus

Maisha Plus - Kipanya
Zikiwa zimebakia wiki takribani mbili kumalizika kwa shindano ya maisha
plus, Mratibu wa shindano hilo Masoud Kipanya, amesema kuwa mpaka sasa
washiriki wameweza kuonyesha uwezo wa hali ya juu katika kukabiliana na
maisha yoyote yale watakayokumbana nayo, hata pindi wataporudi
majumbani kwao baada ya fainali hiyo.


Akiongea na Bongo5,Kipanya amesema kuwa mashindano hayo ya aina yake yameweza kuwafunza namna mbalimbali ambavyo wataweza kukabiliana na maisha yoyote magumu kwani ukweli halisi unajionyesha kutoka katika kijiji hicho cha Maisha plus.

‘Kwa hilo ndugu sidhani kama kuna haja ya kubishana kwani ukweli na hali halisi inajionyesha pale kijijini jinsi vijana wanavyopambana na maisha huku ikiwa ni tofauti kabisa na wao wenyewe walivyotarajia mashindano hayo kuwa” alisema Kipanya.

{seyretpic id=949 align=right}Aidha Kipanya aliendelea kusema kuwa Maisha plus si kama walivyofikiri wengi kuwa pengine vijana hao wangekwenda huko kuonyesha umahairi wao kama vile kuimba,kucheza au hata kuigiza,ila ukweli ni kuwa maisha plus ililenga kuwakumbusha washiriki namna ambavyo maisha ya wazee wetu wa kale yalivyokuwa pamoja na namna ya maisha halali ya mwafrika yalivyokuwa ukiachilia mbali maisha haya ya utandawazi yalioingia kutoka katika nchi za kigeni.

‘Unajua yale na maisha halisi ya sisi waafrika, vijana wanajiafunza hivyo,lengo ni kuionyesha jamii maisha halisi na siyo hali ambayo ipo sasa kwa waafrika wengi wakiwamo watanzania ambao tayari ule utamaduni wao wameusahau na kukimbilia utamaduni toka nje huku chanzo kikubwa kikiwa ni utandawazi”alisema Kipanya.

Mashindano hayo ya Maisha plus yanarushwa hewani na television ya TBC 1 huku pia yakiwa yamedhaniwa na kampuni ya Aurora Security, yalianza kwa kuwashirikisha washiriki wapatao 18 ambapo mpaka sasa tayari jumla ya washiriki 8 wameshayaaga mashindano hayo huku mshindi mmoja akitarajiwa kupatikana katika idadi ya washiriki 10 waliobaki ambapo mshindi huyo atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 10 taslimu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents