DStv Inogilee!

Maisha ya Cardi B na Beyonce yamkosha Linah

Msanii wa Bongo Flava, Linah amesema anavutiwa zaidi na maisha ya Beyonce mara baada ya kuwa mama huku akiendelea na muziki wake kama kawaida.

Muimbaji huyo ambaye pia ni mama wa mtoto mmoja amesema kitu hicho kinamuhasisha kuendelea kufanya muziki.

“Beyonce alijifungua mtoto mmoja na mara ya pili alijifungua watoto mapacha lakini bado akipanda kwenye jukwaa unaweza kusema amepanda mtu ambaye hana mtoto hata mmoja. Ukimwangalia tena Cardi B sasa ana ujauzito mkubwa tu ambao anakaribia kujifungua lakini ebu angalia perfomance yake na the way anavyokwenda,” amesema Linah.

“Kinachonifurahisha ni kwamba hata ile dhana yetu kwamba ukianza tu kuwa na familia umeharibu kwa sababu huwezi kusema wewe ni mwanamuziki usizae, inabidi uwe na familiaa yako na uwe na mume wako lakini uwendelee na kazi yako,” Linah ameiambia XXL ya Clouds Fm.

Tangu Linah alipojifungua ametoa wimbo mmoja uitwao Same Boy ambao ameshirikiana na Recho ukiwa ni mara ya pili kwa wawili hao kukutana katika ngoma moja baada ya kushirikishwa na kundi la Makomando katika ngoma yao inayokwenda kwa jina la Chap Chap.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW