Michezo

Maisha ya nyota wa zamani wa Argentina Diego Maradona kwa picha

Umaarufu wake pekee haumtendei haki,. Diego Maradona alikuwa mchezaji mwerevu kupita kiasi katika uwanja wa mpira na mtu aliyezua utata.

Kutoka nchini anakotoka Argentina hadi ufanisi alioupata Itali, ushindi wake wa kombe la dunia na utumizi wa mihadarati uliomuangusha , tazama maisha yake katika picha.

Diego Maradona mwaka 1982
Maradona alicheza mechi ya fainali ya kombe la dunia akiiwakilisha Argentina mwaka 1982 nchini Uhispania lakini alikuwa maarufu miaka minne baadaye.

Diega Maradona na Peter Shilton wakisalimiana kwa mkono katika kombe la dunia la 1986 kombe la dunia
Kulikuwa na utulivu kabla ya kimbunga: Walisaliamiana kwa mkono na kipa wa England Peter Shilton kabla ya kombe la mechi ya robo fainali ya kombe la Dunia nchini Mexico mwaka 1986

Magoli mawili ya Diego Maradona dhidi ya England katika kombe la Dunia la 1986
Goli la hand of Gold dhidi ya England , lilifuatiwa na goli bora la Karne.

Diego Maradona akishikilia kombe la Dunia
Alikuwa mchezaji wa kivyake: Maradona alitangazwa kuwa mchezaji bora wa FDimba hilo la Dunia baada ya kuisaidia Argentina kupata ushindi 1986, mbali na kuisaidia timu hiyo kufika fainali miaka minne baadaye.

Diego Maradona
Alikuwa mfalme: Maradona alikuwa mchezaji nyota na maarufu katika klabu ya Naoli nchini Itali ambapo alijishindia Kombe la Uefa mwaka 1989 pamoja na mataji mawili ya ligi. Tishati Nambari 10 ilihifadhiwa kwa niaba yake

Diego Maradona mwaka 2001
Maradona, katika picha hii ya 2001, alitatizika na utumizi wa dawa za kulevya na masuala ya kuongeza uzito

Lionel Messi na Diego Maradona
Maradona, akiwa kocha wa taifa wa Argentina akitoa hekima yake kwa mshambuliaji Lionel Messi katika kombe la Dunia la 2010 ambapo walishindwa kwa magoli 4-0 na Ujerumani katika awamu ya robo fainali

Diego Maradona nchini Russia
Maradona akipiga picha na bango la picha yake wakati ambapo timu yake ya taifa Argentina ilikuwa ikicheza dhidi ya Nigeria katika kombe la Dunia lililoandaliwa Urusi 2018.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents