Habari

Maiti 7 zimepatikana katika ajali ya meli ya jeshi la Marekani

Mabaharia saba wamepatikana wakiwa wamefariki dunia baada ya meli ya jeshi la Marekani ilipogongana na meli ya mizigo ambayo ilikuwa na bendera ya Ufilipino katika maeneo ya bahari ya Japan.


Picha ya meli ya kijeshi ya Marekani iliyogongana na meli ya mizigo

Maiti hizo zilipatikana ndani ya meli katika chumba cha kulala ambacho kiliharibika na kujaa maji.


Waokoaji wakiwa katika kazi ya kuokoa katika ajali hiyo

“This loss is something we all feel. We have found a number of the remains … of our missing shipmates, and our deepest sympathies go out to the families of those shipmates,” afisa mmoja wa jeshi a maji la Marekani ameiambia CNN.

Meli ya mizigo ilikuwa ni aina ya ACX Crystal iliyokuwa na urefu wa mita 222 na meli ya kijeshi ya Marekani ina urefu wa mita 154 ambayo pia huwa inatumika katika kuharibu makombora.

Mmoja kati ya makamanda wa jeshi la Marekani alijeruhiwa katika ajali hiyo na alikimbizwa haraka hospitalini usafiri wa helikopta.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents