Habari

Maiti ya kichanga yaokotwa nje ya grosari

Maiti ya mtoto mchanga, imeokotwa nje ya grosari moja maarufu kama `Zero` iliyo jirani na kituo kikuu cha polisi, eneo la Kanyenye mjini hapa.

Na Lucas Raphael, PST, Tabora

 
Maiti ya mtoto mchanga, imeokotwa nje ya grosari moja maarufu kama `Zero` iliyo jirani na kituo kikuu cha polisi, eneo la Kanyenye mjini hapa.

 

Watu walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa waliona watoto wa shule wamejazana katika kontena la kuhifadhia taka wakiangalia mwili wa kichanga hicho.

 

Walisema wanafunzi hao waliokuwa wakishangaa mwili huo walikuwa wakielekea shuleni majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi.

 

Maiti hiyo ilichukuliwa na kupelekwa katika hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete.

 

Wakazi hao waliahidi kusaidiana na Jeshi la Polisi kumsaka aliyefanya unyama huo ili akamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, ili iwe fundisho kwa wengine.

 

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Bw. Muhud Mshihiri alisema polisi wanaendelea kumsaka mwanamke aliyekitupa kichanga hicho.

 

Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents