Habari

Majaliwa awataka watanzania kuchangamkia fursa Dodoma

Baada ya kutimiza ahadi yake ya kuhamia Dodoma, waziri mkuu, Kassim Majaliwa, amewakaribisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kujitokeza kuwekeza na kuchangamkia fursa zitokanazo na serikali kuhamia mjini Dodoma.

1468334510-dsc_0825

Ameyasema hayo jana wakati alipotembelea kiwanda cha kutengeneza magodoro cha Dodoma asili cha mjini humo, Premalt Limited. Aidha alisema serikali imefungua milango kwa wawekezaji wanaotaka kujenga viwanda, nyumba za kuishi, kukodisha kama ofisi masoko makubwa, maeneo ya bustani ya kupumzika na uwekezaji mwingine na serikali itawaunga mkono.

“Ni jukumu lenu Watanzania kuja kuwekeza Dodoma milango iko wazi, serikali hii itawaunga mkono wawekezaji wote wanaotaka kuwekeza Dodoma, wale wanaofikiria serikali haina nia njema na wafanyabiashara wajue hatuhitaji kuweka siasa sana kwenye utendaji,” alisema Majaliwa.

“Hatutaki kuweka siasa sana kwenye utendaji, sehemu kubwa ya ahadi ya Rais John Mgufuli ni kuhakikisha wananchi wanapata tija ya kuhudumiwa na serikali yake tatizo kubwa siasa imewekwa mbele sana,” aliongeza.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kiwanda hicho, Haidary Gulamali, alisema kati ya wafanyakazi 150 walioajiriwa kiwandani hapo, 147 ni Watanzania na watatu ni wataalamu ambao ni raia wa kigeni.

Alisema magodoro ya kiwanda hicho yamekuwa na soko zuri kutokana na ubora wake.

Si mara ya kwanza kwa waziri mkuu Kassim Majaliwa kuwakumbusha watanzania kuchangamkia fursa zitakazopatikana mjini humo.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents