Habari

Majaliwa: Marufuku mwanafunzi kwenda shule peku na nguo zilizochakaa

Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa, amepiga marufuku wanafunzi kuvaa nguo zilizochakaa au kwenda shule wakiwa peku.

2wanafunzi-walemavu-wa-hakili-shule-ya-msingi-namtumbo-mahudhurio-ya-wanafunzi-hawa-yanasemekana-kuwa-ni-hafifu-sana-kutokana-na-kukosa-chakula-shuleni

Ametoa maagizo hayo hivi karibuni akiwa katika ziara yake mjini Kibiti, Pwania wakati akizungumza na wananchi wa eneo hilo kwenye mkutano wa hadhara.

“Zile fedha mlizokuwa mnatumia kulipa ada na michango sasa zitumieni kununua sare na chakula cha watoto wenu, ni marufuku mtoto kwenda shule huku akipekua au akiwa amevaa sare zilizochanika,” alisema Majaliwa.

Pia aliagiza watoto wote wenye umri wa kwenda shule wafanye hivyo.

“DC kuanzia sasa anza msako wa watoto wote wasioenda shule, ili wazazi wao wakamatwe na kuchukuliwa hatua zinazostahili, serikali imetoa fedha ili watoto wetu wasome, na ni marufuku kuozesha mtoto wa kike, mzazi ukihusika tunakukamata na kukufunga, wewe nawe uliyeoa ni jela, hatuna mzaha kwenye hilo,” alisisitiza

Aliendelea kwa kuonya,” Wazazi wenye tabia ya kuozesha watoto kwa kuwakatiza masomo waache mara moja, kwani kuanzia sasa atakayebainika kukatisha masomo ya mwanafunzi hususan wa kike, ajiandae kwenda jela miaka 30.”

Serikali ya awamu ya tano imefuta ada kwenye shule za msingi na sekondari za serikali kama hatua ya kuinua kiwango cha elimu.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents