Habari

Majambazi wafunga mtaa wapora milioni 11/-

MAJAMBAZI sita juzi walifunga mtaa wenye maduka mengi katika kijiji cha Kakonko wilayani Kibondo mwishoni mwa wiki na kupora Sh milioni 11 baada ya kufyatua risasi takriban 50 hewani kuwatisha wananchi, polisi wamethibitisha.

Fadhili Abdallah, Kigoma

 

MAJAMBAZI sita juzi walifunga mtaa wenye maduka mengi katika kijiji cha Kakonko wilayani Kibondo mwishoni mwa wiki na kupora Sh milioni 11 baada ya kufyatua risasi takriban 50 hewani kuwatisha wananchi, polisi wamethibitisha.

 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, Patrick Byatao alisema kuwa majambazi hao wakiwa na bunduki ya SMG walifyatua risasi zipatazo 46 hewani kabla ya kupora. Akisimulia tukio hilo kutoka Kakonko mwananchi mmoja, Essau Eliud alisema kuwa aliona watu karibu wanane wakiwa na bunduki ambao walihusika na tukio hilo.

 

Shuhuda huyo alisema kuwa katika tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita saa 7:30 usiku kijijini hapo, hakuna mtu aliyeuawa au kujeruhiwa licha ya risasi nyingi kupigwa hewani na majambazi hayo.

 

Polisi wamewataja wafanyabiashara walioporwa kuwa ni Francis Zawadi, Kadundus John, Musa Mateso na Simon Kakira na kwamba hadi sasa hakuna mtu yoyote aliyekamtwa kuhusiana na tukio hilo na polisi wanaendelea na msako kuwatafuta majambazi hao.

 

Katika tukio jingine Kamanda Byatao alisema kuwa katika kijiji cha Kagezi wilayani Kibondo karibu na mpaka wa Tanzania na Burundi, polisi wamemtia mbaroni raia mmoja wa Burundi akiwa na bomu la kurushwa kwa mkono.

 

Byatao alisema kuwa mtuhumiwa alikamatwa usiku siku hiyo na alipohojiwa alisema kuwa ni mpiganaji wa Chama cha FNLPalipehutu.

 

Alisema kuwa mpiganaji huyo wa kikundi cha waasi wa Burundi alikuwa anataka kuliuza bomu hilo ili kuweza kupata chakula kutokana na kukabiliwa na ukata hasa baada ya kukataa kujiunga na jeshi la Serikali ya Burundi.

 

Hata hivyo polisi walikataa kutaja jina la mtuhumiwa huyo kwa kile kilichoelezwa kwamba uchunguzi juu ya suala hilo bado unaendelea. Akisimulia tukio hilo kutoka Kakonko mwananchi mmoja, Essau Eliud alisema kuwa aliona watu karibu wanane wakiwa na bunduki ambao walihusika na tukio hilo.

 

Source: Habari Leo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents