Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Majambazi wamwibia hakimu kila kitu

MAJAMBAZI wamevamia nyumba ya Hakimu Mkazi na Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi la Mkoa wa Mbeya, Bibi Hellen Riwa na kupora kila kitu kilichokuwamo ndani ya nyumba yake.

Na Thompson Mpanji, Mbeya


MAJAMBAZI wamevamia nyumba ya Hakimu Mkazi na Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi la Mkoa wa Mbeya, Bibi Hellen Riwa na kupora kila kitu kilichokuwamo ndani ya nyumba yake.


Tukio hilo lilitokea wiki iliyopita usiku wa manane, katika eneo la Pambogo, kata ya Iyela jijini hapa baada ya majambazi hao kubomoa vigae vya paa la nyumba na kuingia ndani.


Ilidaiwa juzi kuwa kabla ya kuingia walimgongea mlango wa chumba msichana wa kazi, Mati Philemon, na baada ya kufungua walimkamata na kumchapa viboko na kumwamuru arudi katika chumba chake na wao kumfungia.


Habari zaidi zilidai kuwa baada ya hapo majambazi hao waliingia jikoni na kupika chakula na kula na kisha kukusanya samani zote zilizokuwa ndani na kupakia katika gari walilotumia ambalo halikuweza kufahamika na kuchoma kumbukumbu muhimu.


Akizungumzia tukio hilo, Bibi Riwa alisema wakati majambazi hao wanavamia nyumba yake yeye alikuwa safarini Tanga kikazi na alipigiwa simu ya kumfahamisha tukio hilo na hivyo kulazimika kukatisha shughuli zake na kurejea hapa.


Hakimu huyo ambaye amehamishiwa katika kituo chake kipya cha kazi hivi karibuni, alisema baada ya kurejea nyumbani, alikuta kila kitu kimehamishwa na majambazi hao na kuchomwa nyaraka zake zote ikiwamo hati ya kusafiria, barua ya ajira, stakabadhi alizonunulia samani za ndani na kumbukumbu nyingine muhimu.


Bibi Riwa alivitaja baadhi ya vitu hivyo kuwa ni pamoja na l uninga, makochi, magodoro, masanduku 10 ya nguo mbalimbali na samani zote za ndani ambapo waliharibu dishi baada ya kushindwa kulibeba na kwamba thamani ya mali hizo bado haijajulikana kutokana na stakabadhi zote kuchomwa moto.


Source: Majira

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW