Majambazi yapora Gapco Magomeni

Majambazi wanne jana saa 3:00 asubuhi walivamia kituo cha mafuta cha Gapco, kilicho katika makutano ya Barabara ya Morogoro na Kawawa umbali wa hatua zisizozidi 150 kutoka kituo cha polisi cha Magomeni.

SASA ni dhahiri; wimbi la ujambazi limerudi upya baada ya kutulia kwa muda mrefu.

Majambazi wanne jana saa 3:00 asubuhi walivamia kituo cha mafuta cha Gapco, kilicho katika makutano ya Barabara ya Morogoro na Kawawa umbali wa hatua zisizozidi 150 kutoka kituo cha polisi cha Magomeni, na kumpiga risasi mhasibu wa kituo hicho cha mafuta kabla ya kupora mamilioni ya fedha na kutoweka.

Tukio hilo la uporaji wakati jua likiwa limeshashamiri, ukiacha matukio ya kuteka vijiji, mabasi na masoko, ni salamu tosha kwa Jeshi la Polisi kwamba wimbi la ujambazi lililokuwa likifanyika waziwazi katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, sasa limerudi upya.

Matukio ya ujambazi yalikuwa yametulia tangu serikali ilipoamua kufanya operesheni maalum ya kupambana na uhalifu huo, ikiongeza askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kufanya doria barabarani na kutumia pikipiki kudhibiti nyendo za majambazi, hatua ambayo ilikuwa na mafanikio makubwa.

Lakini jana, majambazi yaliyovamia kituo hicho cha mafuta yalionekana kurudia ukatili wao wa kuua wakati yalipokuwa yamepania kupora fedha za kituo hicho ambazo zinasadikiwa kuwa ni mauzo ya siku nne.

Mashuhuda wanasema risasi kadhaa zilipigwa hewani na majambazi wawili, wakati wenzao wakiwa wamevamia kituo hicho.

Majambazi hayo, kwa mujibu wa mashuhuda, walitinga kituoni hapo wakiwa na gari aina ya Toyota Mark ll. Wakionekana kuwa walishajua nyendo za mhasibu, majambazi hayo yalizuia gari lililomchukua mhasibu huyo, Seraphine Madenge na mkurugenzi wa kituo hicho, George Kretson, 74 ambaye ni raia wa Ugiriki, na kulisimamisha.

Baadaye, kwa mujibu wa mashuhuda hao, jambazi mmoja alishuka na kwenda kugonga kwenye kioo cha gari hilo na alipoona hawafungui ndipo alipokivunja kwa ngumi na baadaye kuomba apewe fedha. Alipokataa ndipo walipomuua mhasibu huyo kwa risasi.

Mmoja wa walinzi wa eneo hilo, aliyeomba jina lake lisitajwe gazetini, alisema majambazi hao walimuua mhasibu huyo katika kujibu mapigo baada ya mlinzi mmoja kufyatua risasi hewani katika kutaka kuwazuia wasitekeleze nia yao.

“Mlinzi mwenzangu ambaye analinda kituo hiki cha mafuta baada ya kuona majambazi hao wanalizuia gari la mkurugenzi, akahisi kuna hali ya hatari na akaanza kupiga risasi hewani bila kujua kama maadui hao wana silaha ama

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents