Habari

Majambazi yavamia hoteli za kitalii

WATU wanaoshukiwa kuwa majambazi wamewajeruhi watu wawili na kumuua mbwa kwa kuwapiga risasi. Tukio hilo lilitokea juzi usiku baada ya watu hao, kuvamia hoteli mbili za kitalii zilizopo eneo la Paje Mkoa wa Kusini Unguja.

Na Salma Said, Zanzibar

 

 

 

WATU wanaoshukiwa kuwa majambazi wamewajeruhi watu wawili na kumuua mbwa kwa kuwapiga risasi.

 

 

 

Tukio hilo lilitokea juzi usiku baada ya watu hao, kuvamia hoteli mbili za kitalii zilizopo eneo la Paje Mkoa wa Kusini Unguja.

 

 

 

Akizungumza kwa simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Amin Mahamba alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 2:00 usiku.

 

 

 

Kamanda Makamba, alisema katika kikundi cha watu sita waliokuwa na silaha za kivita, kiliingia katika eneo la Hoteli ya Cristal na Kinazi Upepo, kuanza kupiga risasi hewani.

 

 

 

 

 

Alisema wakati wengine wakifyatua risasi hewani, mmoja wao, alimpiga mbwa ambaye alikuwa akimbweka kuashiria hali ya hatari.

 

 

 

Alisema baadaye, waliwageukiwa watu wawili ambao walikuwa karibu na eneo la hoteli hizo na kuwajeruhi.

 

 

 

Kamanda huyo aliwataja majeruhi hao ambao wamelazwa katika Hospitali na Mnazi Mmoja ni Hassan Khamis, wa Zanzibar na mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Jonathan, Raia wa Kenya aliyekuwa na mkewe Muingereza.

 

 

 

Kamanda huyo, alisema thamani ya mali zilizoporwa bado haijajulikana, lakini

 

inakisiwa kuwa ni za zaidi ya Sh2 milioni.

 

 

 

Baadhi ya mali zilizoporwa katika tukio hilo kuwa ni simu za mkononi na kamera za wageni.

 

 

 

Uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo, unaendelea na taarifa kamili zitatolewa baada ya kukamilika.

 

 

 

Kufuatia tukio hilo, ulinzi uliimarishwa katika maeneo hayo chini ya ufadhili wa wamiliki wa hoteli za kitalii katika ukanda wa Utalii kwa kushirikiana na Polisi, Kamisheni ya Utalii Zanzibar na Vyombo vya Dola.

 

 

 

Wimbi la ujambazi wa kutumia silaha za moto hivi sasa linaonekana kukua kwa kasi

 

katika Mikoa ya Kusini na Kaskazini Unguja ambako watalii wengi nyakati za usiku

 

hurejea katika hoteli walizofikia.

 

 

 

Imebainika kuwa, majambazi wamekuwa wakivizia kwenye sehemu wanazopita na kuwanyang’anya vifaa vyao ikiwamo simu, kamera na mabegi ya nguo.

 

 

 

Source: Mwananchi

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents