Fahamu

Majaribio ya chanjo ya Covid-19 kuanza tena

Majaribio ya chanjo ya corona yameanzishwa tena baada ya zoezi hilo kusimamishwa kwa muda mfupi. Wakati huo huo idadi ya maambukizi inaendelea kuongezeka katika nchi kadhaa kote ulimwenguni.

Coronavirus Impfstoff Symbolbid (picture-alliance/Flashpic)

Matumaini ya kupata afueni kutokana na janga la corona duniani kote yalididimia mapema wiki hii wakati kampuni ya dawa ya AstraZeneca na Chuo Kikuu cha Oxford cha nchini Uingereza zilipotangaza kuwa zimesitisha majaribio ya chanjo hiyo baada ya mtu aliyejitolea kutoka Uingereza kupata ugonjwa ambao haueleweki.

Lakini hapo Jumamosi 12/09/2020 majaribioya chanjo hiyoyalipewa ruhusa ya kuanza tena na wasimamizi wa Uingereza baada ya chanjo hiyo kufanyiwa ukaguzi na kudhihirishwa kuwa ni salama. Kampuni ya dawa ya AstraZeneca pia imetangaza kwamba itaanza tena majaribio ya chanjo hiyo huko nchini Brazil baada ya kupewa ruhusa.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya dawa ya AstraZeneca Tom Mc Killop.Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya dawa ya AstraZeneca Tom Mc Killop.

Huku mamilioni ya watu wakiwabado wanakabiliwa na athari za maambukizi ya corona na ugonjwa wa COVID -19, mbio za kutafuta chanjo ulimwenguni koteĀ  zinaendelea. Kampuni tisa tayari zikiwa katika awamu ya tatu ya majaribio ya chanjo ya corona.

Kampuni ya AstraZeneca amesema ina matumaini kwamba chanjo inaweza kupatikana hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu au mwanzoni mwa mwaka ujao. Chuo Kikuu cha Oxford kimesema katika majaribio makubwa kama haya, inatarajiwe kwamba baadhi ya washiriki watakuwa wagonjwa na kwamba kila tukio lazima lichunguzwe kwa uangalifu.

Mhadhiri wa matibabu ya wagonjwa mahututi katika Chuo Kikuu cha Cambridge, Charlotte Summers, amesema kusimamishwa kwa majaribio ya chanjo hiyokwa muda mfupi inaonyesha nia ya dhati ya watafiti ya kulipa kipaumbele suala la usalama katika mpango huo wao wa maendeleo.

Amesema ili kukabiliana na janga la COVID -19 linaloukabili ulimwengu mzima, inahitajika kupatikana chanjo na tiba ambazo watu hawatakuwa na wasiwasi kuzitumia.

Chanzo:/AFP

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents