Habari

Majeruhi 3 wa shule ya Lucky Vincent kutibiwa Marekani

Majeruhi watatu wa ajali iliyosababisha vifo vya wanafunzi na walimu pamoja na dereva wa shule ya Lucky Vicent wa jijini Arusha, ambao walikuwa wakipatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru, wanatarajia kupelekwa Marekani kwa Matibabu zaidi.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya mkoa Arusha, Dkt Timoth Wonanji amesema hali za majeruhi hao zinaendelea vizuri na kwasasa hawana maumivu makali kama hapo awali.

Madaktari bingwa kutoka Marekani wamejitolea kutoa huduma ya matibabu bure kwa wanafunzi hao. Insemekana madaktari hao kutokea Marekani, walikua wakielekea Ngorongoro walipokutana na ajali hiyo Karatu ambapo walihusika kutoa huduma ya kwanza katika eneo la ajali hiyo.

“Wameona ni vyema wakajitolea watoto hawa wapate matibabu zaidi nje ya nchi, kwahiyo kwasasa hivi tunachokifanya tupo kwenye hatua za awali ambapo tumewafanyia uchunguzi hali zao zipo stable, wanaweza wakasafiri kwenda nje ya nchi ili waendelee kupata matibabu zaidi,” alisema Dkt Wonanji.

Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyarandu ameeleza jinsi madaktari hao walivyojitolea “Hospitali kuu ya Mercy Hospitali imekubali kuwapokea na kuwatibu hawa watoto wote bure kwa maneno mengine watatoa dawa, watato madaktari bingwa wa aina zote mifupa nakadhalika kwa kila mtoto na Bwana Mrisho Gambo amefanya kazi kubwa sana kwa kuhakikisha kwamba utaratibu wa kuwapatia pass za kusafiria kina mama watatu ambao wataenda na watoto wao, uko katika hatua za mwisho either leo usiku au kesho asubuhi tunatarajia kwamba waende Dar es salaam wapatiwe pass za kusafiria.”

Hata hivyo, wazazi wa watoto hao wameshukuru kwakuwa watoto wao wanaendelea vizuri.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents