Habari

Majibu baada ya Rais Trump kupimwa afya ya akili

Kufuatia uchunguzi wa kiafya uliofanywa na daktari wa White House umeeleza kuwa Rais Donald Trump hajaonyesha dalili zozote za matatizo ya kiakili.

Rais Trump akisalimiana na Dkt Jackson

Kufuatia uchunguzi wa kiafya uliofanywa na daktari wa White House umeeleza kuwa Rais Trump hajaonyesha dalili zozote za matatizo ya kiakili.

Wiki iliyopita Trump alifanyiwa uchunguzi wa afya kwa saa tatu, hii ni baada ya kutolewa kitabu chenye utata ‘Fire and Fury’ kulichoeneza uvumi kuhusu afya ya kiakili ya Rais Trump.

Akiongea na waandishi wa habari wakati wa mkutano huko White House, Dkt Ronny Jackson alisema kuwa kwa jumla afya ya rais huyo ni nzuri.

” Sina wasi wasi wowote kuhusu afya ya akili ya Trump, anaendelea kufurahia moyo wenye afya na afya yote kwa jumla kutokana na kutovuta sigara na kutokunywa pombe,” alisema Dkt Jackson.

Hata hivyo Dkt Jakcson alisema kuwa Rais Trump 71, atanufaika kwa kupunguza vyakula vyenye mafuta na mazoezi zaidi.

Hata hivyo Rais Trump amemjibu mwandishi wa kitabu cha Fire and Fury, Michael Wolf kwa kusema kitabu hicho kimejaa uongo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents