Michezo

Simba nikumbukeni kwa mabaya yangu, mazuri yaacheni – Kaseja

Mlinda mlango wa zamani wa Taifa Stars na Simba, Juma Kaseja ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Mbeya City, ana historia nzuri ndani ya klabu ya Simba kwani ni miongoni mwa magolikipa mahiri waliowahi kuidakia timu hiyo kwa mafanikio makubwa.

kaseja

Hata hivyo Jumatatu hii, kupitia account yake ya Instagram, Kaseja aliandika ujumbe ambao kwa mara moja ni ngumu kuelewa alimaanisha nini lakini ulikuwa na maana kubwa.

“Wana ssc nikumbukeni kwa mabaya niliowafanyia kwenye timu yenu mazuri yaacheni,” aliandika.

kas

Bongo5 ilimtafuta Juma Kaseja na haya ndio yalikuwa majibu yake:

Hamna huo ni ujumbe tu kila anayefikiria acha abaki hivyo hivyo na maswali tu ila mimi nafurahia sana maisha ya huku na timu yangu ya Mbeya City.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents