Majibu ya Kamati ya Miss TZ juu ya aliyeshiriki shindano la Miss Africa USA

Jana Bongo5 iliweka habari inayomhusu mtanzania aliekereketwa kwa taarifa ya Maggie Munthali kushiriki mashindano ya kuwania taji la Miss Afrika USA wakati, yeye akidhani, hawajawahi kuonekana katika mashindano yoyote ndani ya Tanzania na kumtuhumu ameilaghai Tanzania kwa kutumia fursa ambayo alitakiwa itumiwe na Miss Tanzania, labda kwa kwa mtazamo wa watanzania angeiwakilisha vizuri Tanzania kwa kuwa ni chaguo la watanzania wote.

Baada ya taarifa hiyo kuwafikia walengwa, kamati ya Miss Tanzania kupitia kwa afisa habari wao, Bwana Aidan Rico wametoa ufafanuzi kwa watanzania, hasa hasa waishio USA kuhusiana na mrembo Maggie Munthali aliyeshiriki shindano la Miss Africa USA.

Katika taarifa yake ambayo aliitoa kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, bibie Maggie aliana safari yake ya kushiriki Miss Tanzania, kuanzia ngazi ya Kitongoji cha Mzizima mwaka 2005. Na baada ya hapo alifanikiwa kuinngia Top 3 ya shindano hilo hivyo kupata nafasi ya kuiwakilisha kitongoji hicho katika ngazi ya kanda ya Ilala kwa mwaka huo.Mrembo huyo hakupata nafasi ya kuingia katika Fainali za Taifa kwa mwaka huo 2005. aliishia ngazi ya Kanda ya Ilala.

ufafanuzi huo unaendelea kwa kusema,Kanda ya Ilala kwa mwaka huo iliwakilishwa na Feza Kessy, Perminda Raj na Lilian Mushi, na mshindi wa mwaka huo alikuwa NANCY SUMARI ambaye pia alitwaa taji la MISS WORLD AFRICA 2005.

Katika taarifa hiyo bwana Rico alitabanaisha kuwa, kamati ya Miss Tanzania haina kipingamizi chochote kwa mrembo huyo kushiriki mashindano mengine yoyote ya urembo mahali popote pale. Kamati inamtakia kila la heri mrembo huyo na wengine watakaojitokeza kutangaza jina la Tanzania katika fani ya urembo.

Tunamnukuu “Hatujui ni vigezo gani walivyotumia hao waandaaji wa shindano hilo la Miss Africa USA, hadi kumpa Jina / sash ya Miss Tanzania, lakini tunaimani tu kwamba ni mrembo anayewakilisha Tanzania ijapokuwa hakuingia katika Fainali za Taifa”. Mwisho wa kunukuu.

Tukiwa kama wadau wa burudani, mitindo, ulimbwende, michezo, muziki na fani nyingine zinazofanana na sanaa tunapenda kuhitimisha suala hili, baada ya kuwa limetolewa ufafanuzi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents