Habari

Majibu ya Waziri Lukuvi kwa walionyang’anywa mashamba

Waziri wa Ardhi,Nyumba,Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema kuwa kama mtu haendelezi shamba lake au kiwanja chake ni sababu tosha ya mtu kunyang’anywa shamba lake.


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi

Waziri Lukuvi ameyasema hayo kipindi cha Mizani cha Azam TWO ambapo pia Waziri Mstaafu Frederick Sumaye aliilalamikia serikali kumnyanga’nya mashamba yake.

“Sio kwamba nia ya mtu au matakwa ya mtu kunyanga’nya ni matakwa ya sheria sasa imejitokeza watu wachache kuchukua ardhi watu wengi wamechukua ardhi sana wengine wa hekari laki moja laki mbili lakini uwiano wa wawekezaji wa ardhi ile wakati wamechukua kwa mfano kuna hati moja hapa hii ambayo wanaipigia pigia kelele tangu mwaka 39 hati lile tangu mwaka 39 imekuwa inatembea tu kwenye mashamba ya watu sasa miaka ile watu walikuwa wachache unapoenda kuchukua eneo la kijiji hekari elfu 60 kwa mfano hivi wananchi umewaachia nini,” alihoji na kueleza Waziri Lukuvi.

“Mara nyingi unapowahi kuchukua eneo hilo kama Morogoro mtu unawahi ardhi inayolimika sasa hekari yote hiyo wewe unachukua hekari elfu 60 alafu huiendelezi alafu shamba hilo tunalikuta bank umelikopea na fedha zile umepata umejengea apartment mahali pengine kule wananchi wanalimezea mate serikali inatumia nguvu sana kuhimiza wananchi wasilivamie lile shamba lako serikali hatupati kodi lakini mbaya zaidi kodi ya ardhi ile ambayo umeikopea hulipi unataka serikali ifanye nini? alihoji.

“Serikali sisi tumekuwa na huruma sana kwa miaka mingi lakini serikali ya awamu ya tano tumekubaliana kufuata sheria kila mtu afuate sheria kwenye kodi tumesimamama kidete kila mahali kila mtu lazima alipe kodi kwahiyo mtu yoyote asielipa kodi ya ardhi ni sababu tosha ya kunyanga’nywa ardhi yake na hati yake kufutwa hilo kila mtu lazima ajue iwe ni kiwanja au ni shamba kama unatabia ya kutokulipa kodi ya ardhi ni haki yetu kisheria kunyanga’nya shamba lako au kiwanja chako na tunafanya hivyo kama shamba huendelezi kiwanja huendelezi ni sababu tosha ya kunyanga’nya shamba lako kwahiyo sababu kubwa ya kunyanga’nywa ni kushindwa kuliendeleza .”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents