Michezo

Majimaji Serebuka Festival watangaza neema kwa wakazi wa Ruvuma

Majimaji Serebuka ni tamasha linalofanyika Songea, Mkoani Ruvuma kila mwaka. Lilianzishwa 2015 na taasisi isiyo ya kiserikali ya SONGEA MISSISSIPPI (SO-MI) ikishirikiana na Kampuni ya Tanzania Mwandi. Mwaka huu litafanyika tarehe 13-20 Julai, 2019, Uwanja wa Majimaji, Songea.

Malengo

  1. Kuongeza wigo wa soko kwa wajasiliamali na wafanyabiashara kupitia maonesho ya biashara;
  2. Kuongeza ufahamu wa masuala mbalimbali kwa wanafunzi wa sekondari;
  3. Kuibua na endeleza vipaji kupitia michezo na ubunifu wa aina mbalimbali mfano uchoraji;
  4. Kushawishi watu mbalimbali kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo mkoani humo, mfano, Luhira Game Reserve, Liparamba Game Reserve, Matogoro Mountain Forests, Mbamba Bay Beach, Majimaji Memorial Museum, German Boma, Ruvuma River Water Falls, Tulila HEP site n.k

Mwaka huu itakuwa ni msimu wa tano kufanyika na linapambwa na kauli mbiu; MTU NI AFYA.

Matukio;

  1. Mbio kwa afya (5km, 100m, 200m na 400m)
  2. Mbio za baiskeli (100km Mbinga-Songea)
  3. Mdahalo wanafunzi wa sekondari
  4. Maonesho ya biashara na ujasiliamali
  5. Ngoma za asili
  6. Utalii wa ndani
  7. Uchoraji
  8. Soka
  9. Kongamano la wafanyabiashara

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents